IEBC inahitaji shilingi bilioni 61 kufanya uchaguzi

  • | Citizen TV
    883 views

    Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC sasa inasema inahitaji shilingi bilioni 61 kuandaa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027, ikisema inalenga kusajili takriban wapiga kura milioni sita. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya sheria ya bunge la kitaifa, naibu afisa mkuu mtendaji wa IEBC Obadiah Keitany alisema IEBC itahitaji kununua vipakatalishi vingine vipya baada ya vilivyonunuliwa miaka kumi iliyopita kupoteza thamani yao.