Kaunti ya Nairobi yaagizwa kuondoa rundo la taka nje ya afisi za kampuni ya umeme

  • | KBC Video
    659 views

    Halmashauri ya kitaifa ya usimamizi wa mazingira -NEMA imeitaka serikali ya kaunti ya Nairobi kuondoa mara moja rundo la taka lililomwagwa nje ya afisi za kampuni ya umeme kwenye jumba la Stima plaza. Kupitia mkurugenzi wa utekelezaji wa halmashauri hiyo Dkt. Ayub Macharia, serikali ya kaunti ya Nairobi ilikosea kwa kujihusisha na vitendo visivyo halali ambavyo vinahatarisha afya ya wakazi. Na kama anavyotuarifu mwanahabari wetu John Kahiro, Haya yanajiri huku shughuli za utoaji huduma katika jumba la Stima plaza zikisitishwa kwa muda kutokana na uvundo unaotokana na rundo hilo la taka.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive