IEBC wataka kutengewa pesa za kuandaa uchaguzi mapema

  • | KBC Video
    48 views

    Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka, inataka sehemu ya fedha za uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutengwa katika bajeti ya mwaka 2025/2026 ili kuiwezesha kuanza maandalizi ya uchaguzi huo mapema. Tume hiyo, iliyofika mbele ya Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Haki na Masuala ya Kisheria, ililiomba bunge kuagiza kutolewa kwa angalau shilingi bilioni 15 ili kuiwezesha kununua vifaa vya kidijitali. Wakati uo huo, Idara ya Maslahi ya Kijamii inataka Bunge kutoa shilingi bilioni 16 kwa ajili ya mpango wa kuwakimu wakongwe kila mwezi ikionya kuwa kucheleweshwa kwa fedha hizo kunaweza kuwafanya wazee kukosa marurupu hayo hayo kuanzia mwezi Machi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive