Tanzania yadhibitisha wagonjwa wa Mpox, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    5,024 views
    Mamlaka ya afya nchini Tanzania imethibitisha kuwepo kwa visa viwili vya ugonjwa wa Mpox. Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imeeleza kuwa wagonjwa hao walibainika baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo, ikiwemo vipele usoni, mikononi, miguuni, na sehemu nyingine za mwili, pamoja na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni, na maumivu ya viungo kama misuli na mgongo.