Angola yasema itajaribu kusimamia mazungumzo kati ya DRC na M23
Angola imesema siku ya Jumanne itajaribu kusimamia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika siku zijazo.
Haikufahamika iwapo serikali ya Congo, ambayo ilikataa mara nyingi kufanya mazungumzo na M23, itashiriki katika mazungumzo hayo.
Msemaji wa ofisi ya rais wa Congo aliiambia Reuters mamlaka hiyo imezingatia hatua hiyo, wakati naibu msemaji wa M23 alisema ulikuwa “ni ushindi wa hoja” na kuthibitisha ushiriki wa kikundi hicho katika mazungumzo hayo.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi alifanya ziara ya kikazi mjini Luanda na alikutana na mwenzie Joao Lourenco, ofisi ya rais wa Angola ilisema katika taarifa kwenye Facebook.
“Angola kama mpatanishi katika mzozo wa mashariki mwa Congo, itaanzisha mawasiliano na M23, ili wajumbe kutoka Congo na M23 wafanye mazungumzo ya moja kwa moja mjini Luanda katika siku zijazo,” ofisi ya rais iliongeza.
Nchi hiyo iliyoko Kusini mwa Afrika imekuwa ikijaribu kusimamia kufikiwa kwa sitisho la mapigano na kupunguza mivutano kati ya Congo na jirani yake Rwanda, ambayo imekuwa ikishutumiwa kuwasaidia kikundi cha waasi wa Kitutsi.
Rwanda imekanusha kuwapa msaada wa silaha na wanajeshi waasi wa M23, na imesema majeshi yake yanajihami dhidi ya jeshi la Congo na wanamgambo wenye chuki na Kigali.
Waasi wa M23 wamekamata miji mikubwa miwili iliyoko mashariki mwa Congo tangu Januari katika mvutano wa mgogoro wa muda mrefu ambao kiini chake ulisambaa Congo kutokana na mauaji ya halaiki ya Rwanda yam waka 1994 na juhudi ya kutaka kudhibiti eneo kubwa lenye madini nchini Congo.
#angola #waasi #m23 #congo #felixtshisekedi #JoaoLourenco #rwanda
14 Mar 2025
- This is a major change compared to the previous 8-4-4 curriculum.
14 Mar 2025
- The announcement comes amidst ongoing KCSE registration
14 Mar 2025
- The families of the victims have been waiting for almost two years to bury their loved ones and find closure.
14 Mar 2025
- Bribery allegations have rocked the Machakos County Assembly after the majority's appointment committee approved Annastacia Munyaka's nomination as CEC for Water and Sanitation.
14 Mar 2025
- Police in Muhoroni Sub-county, Kisumu County are investigating the brutal murder of a 17-year-old female Form Four student whose decomposing body was found dumped in a sugarcane plantation in Migingo area.
14 Mar 2025
- U.S. President Donald Trump on Thursday threatened to slap a 200% tariff on wine, cognac and other alcohol imports from Europe, opening a new front in a global trade war that has roiled financial markets and raised recession fears.
14 Mar 2025
- This comes after Kenya hosted the RSF and its allies who signed a pact to form a parallel government.
14 Mar 2025
- Twelve people have been confirmed dead following a tragic road accident at Migaa area on the Nakuru-Eldoret Highway.
14 Mar 2025
- Among the recommendations put forward was the establishment of legal and policy reforms to address the issue.
14 Mar 2025
- A British jury on Thursday convicted a United Nations judge of forcing a young woman to work as a slave after tricking her into coming to the U.K.
14 Mar 2025
- This is a major change compared to the previous 8-4-4 curriculum.
14 Mar 2025
- Ridiculous Ruto
14 Mar 2025
- I've no regrets if I'm sacked, says CS Muturi