Baadhi ya wawakilishi wadi wajeruhiwa kwenye zogo katika bunge la kaunti ya Machakos

  • | Citizen TV
    100 views

    Kizaazaa kimezuka katika bunge la kaunti ya Machakos ambapo baadhi ya wawakilishi wadi wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitalini. vurugu zilizuka baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu hatua ya kumtimua mamlakani spika wa bunge hilo Anne Kiusya huku kundi jingine likitaka kuanzisha hoja ya kumg'oa mamlakani gavana Wavinya Ndeti. Aidha, hoja ya kumtimua kiongozi wa wachache bungeni humo Mbili Wa Ndawa ilikuwa ijadiliwe kabla ya zogo kutibuka. maafisa wa polisi wamezingira majengo ya bunge la kaunti ya Machakos kudumisha usalama, huku shughuli zote zikisitishwa kwa sasa.