Maafisa wa polisi waanza kupiga doria Marigat-Chemolingot

  • | Citizen TV
    448 views

    Maafisa wa usalama katika kaunti ya baringo wameanzisha doria kwenye barabara ya Marigat kuelekea Chemolingot ili kukabiliana na visa vya mashambulizi dhidi ya magari ya wafanyabishara . Akizungumza na wanahabari, kamanda wa polisi kwenye kaunti hiyo Julias Kiragu amesema katika kipindi cha wiki moja iliyopita, visa vitatu vya magari kushambuliwa kwa risasi vimeripotiwa. Aidha kiragu ametoa hakikisho kwamba maafisa wa usalama watawakabili wahusika wa mashambulizi hayo kwani tayari wana taarifa muhimu kuwahusu na kuwa ni vijana wenye umri mdogo.