Viongozi wa Mombasa wataka ubomoaji usitishwe

  • | Citizen TV
    2,206 views

    Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Mombasa wameitaka serikali kusitisha ubomoaji wa zaidi ya makazi 1,000 eneo la Changamwe. Hali hiyo imezua taharuki na wasiwasi miongoni mwa wakazi hasa katika mitaa ya Migadini, Lilongwe na Port Reitz. Kulingana na wakazi baadhi ya mabwenyenye na wanasiasa walioko serikalini ndio wanaoshinikiza ubomoaji huo ili kuwekeza katika eneo hilo. Akizungumza katika eneo hilo, mbunge wa changamwe omar mwinyi ametaka serikali itafute suluhu ya haraka ya mzozo wa shamba hilo.