Dosari za bajeti ya Busia

  • | Citizen TV
    251 views

    Huku wakazi wa kaunti ya Busia wakisubiri bunge la kaunti hiyo kupitisha bajeti ya ziada ya mwaka wa kifedha wa 2025/2026, huenda kaunti hiyo ikazidi kusalia nyuma iwapo dosari zinazoshuhudiwa kwenye bajeti hiyo hazitatatuliwa. Kamati ya ushauri katika maswala ya bajeti na uchumi huko busia kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii ndiyo imefichua hayo, kaunti hiyo ya mpakani ikiwa miongoni mwa zile zilizosalia nyuma na zilizo na kiwango cha juu cha umasikini.