Wawakilishi wadi watatu wajeruhiwa kwenye kizaazaa bungeni Machakos

  • | Citizen TV
    1,201 views

    Kizaazaa kilishuhudiwa mchana kutwa katika bunge la kaunti ya Machakos baada ya waakilishi wadi wanaomuunga mkono spika Anne Kiusya kutofautiana na wale wanaompinga. Yote haya yalianza wakati wa mkutano ndani ya ofisi ya spika ambapo pande mbili zilizozana na kusababisha kujeruhiwa kwa wawakilishi wadi kadhaa.