Walinzi wawili wa Justin Muturi waondolewa

  • | Citizen TV
    5,951 views

    Haya yalipokuwa yakijiri, aliyekuwa waziri wa utumishi wa umma Justin Muturi naye sasa anasema walinzi wake wameondolewa na serikali. Muturi akisema kuwa hatua hii inatokana na kuendelea kwake kumkashifu rais William Ruto. Spika huyu wa zamani anafaa kuwa na walinzi wawili kama mojawapo ya marupurupu ya kikatiba ya nafasi aliyoshikilia awali hata hivyo anasema hatatishwa akiendeleza madai kuwa ikulu ya Nairobi ni uwanja wa ufisadi.