Simba vs Al Masry : Je, Simba ya Tanzania itaivunja laana ya Mwakarobo?

  • | BBC Swahili
    1,912 views
    - "Simba ajiandae kutoka, abakie Mwakarobo, tuendele kubakia na lile jina, na pale Mwakarobo hawezi kutoka, ni Mwakarobo, nusu haiwezekani, Simba uwezo hana." - Katika soka la Tanzania, majibizano ya mashabiki wa Yanga na Simba si jambo geni, lakini jina la "Mwakarobo" limejikita zaidi katika simulizi ya maumivu ya mara kwa mara ya Simba kutolewa kwenye hatua ya robo fainali. Mwakarobo ni jina la kawaida tu la asili ya watu wa Mkoa wa Mbeya, hasa Tukuyu. - Leo tarehe 9 Aprili 2025, Simba itaingia dimbani Benjamin Mkapa kurudiana na Al Masry, ikiwa na lengo moja: Kufuta jina hilo kwa nguvu ya mabao, kushinda kwa zaidi ya mabao matatu na kuvuka hadi nusu fainali ya tatu katika historia yao ya mashindano ya Afrika. Je, safari hii itafanikiwa kuivunja laana ya Mwakarobo? - - - #simba #simbasctanzania #mnyama #tanzania #kandanda #bbcswahili #MICHEZOSubscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw