Uhaba wa Walimu Kutishia Elimu ya Sekondari ya Juu

  • | K24 Video
    44 views

    Huenda masomo yakakumbwa na changamoto kubwa katika shule za sekondari ya juu ifikapo mwaka ujao kutokana na uhaba wa walimu. Serikali sasa inatakiwa kuwekeza zaidi katika utekelezaji wa mtaala wa CBC, ambao umekumbwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kutosha kwa baadhi ya masomo mapya. Wadau wa elimu wanatoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha kuwa wanafunzi hawataathirika.