Ajifungua baada ya kupandikiza tumbo la uzazi la dada yake

  • | BBC Swahili
    1,326 views
    Mtoto wa kike anayechukuliwa kuwa wa "muujiza" amekuwa wa kwanza nchini Uingereza kuzaliwa na mama kupitia njia ya kupandikizwa kwa kizazi. Mama wa mtoto huyo, Grace Davidson, 36, alizaliwa na shida katika tumbo la uzazi, na dada yake akamsaidia tumbo lake mwaka 2023 katika kile ambacho wakati huo kilikuwa upandikizaji pekee wa uzazi uliofaulu nchini Uingereza. Tangu wakati huo, karibu upandikizaji wa aina hii 135 umefanywa katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marekani, China, Ufaransa, Ujerumani, India na Uturuki na Takriban watoto 65 wamezaliwa. #bbcswahili #uingereza #uzazi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw