KEPSHA: Walimu wakiongezewa kazi, pia waongezewe pesa

  • | Citizen TV
    157 views

    Uongozi wa Muungano wa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi nchini Kenya (KEPSHA) umeitaka serikali kuwapandisha daraja walimu wakuu ambao wamekwama katika vikundi sawa vya kazi licha ya kuongezewa majukumu. Akizungumza katika kongamano la kila mwaka la KEPSHA lililofanyika Migori, Mwenyekiti wa KEPSHA, tawi la nyanza Elly Ondiek, alisisitiza kwamba kuanzishwa kwa mtaala mpya wa CBC kulileta majukumu mengi ya ziada kwa walimu, lakini malipo yao hayakuambatanishwa na kazi zao. Ondiek alisema kuwa kazi za ziada walizopewa walimu zinapaswa kuwiana na malipo.