Vijana wapewa mafunzo maalum ya ufugaji wa Samaki Pamoja na vifaa vya uvuvi

  • | Citizen TV
    95 views

    vijana zaidi ya 200 katika Kaunti ya Tana River wamepata msukumo mkubwa katika azma yao ya kupambana na changamoto zinazokabili biashara za uchumi wa baharini katika kaunti hiyo. Kupitia kwa Mpango wa BlueBiz, wataalam mbalimbali wamewafunza vijana hao jinsi ya kufuga samaki, kubashiri soko na vile vile kufikisha bidhaa zao katika masoko yenye uhitaji. Kadhalika vijana hao wamepewa zana za uvuvi ili kupiga jeki sekta hiyo.