Kampuni ya usambazaji maji Malindi MAWASCO inakadiria hasara kutokana na wizi

  • | Citizen TV
    116 views

    Kampuni ya usambazaji Maji mjini Malindi MAWASCO inakadiria hasara kutokana na idadi kubwa ya wakazi wanaotumia njia za mkato kupata maji. Msimamizi wa MAWASCO, John Njoroge, anasema kuwa kiwango kikubwa Cha Maji kinachonunuliwa na kaunti hiyo kutoka kwa Kampuni ya maji ya Coast Water hulipia na wakazi huku asilimia arobaini ya maji hayo ikiishia kwenye wateja wanaojiunganishia Maji bila kufuata taratibu.Baadhi ya watu ambao wanajihusisha na uwizi huo wa maji ni wamiliki wa hoteli, majengo ya biashara na watu wenye majumba ya kifahari katika mji huo wa kitalii.