Wanahabari na wafanyikazi wa Huduma Centre watoa damu Mombasa

  • | Citizen TV
    393 views

    Huku taifa likiendelea kushuhudia uhaba wa damu, muungano wa waandishi wa habari chini ya mwavuli wa Coast Media, na wafanyikazi katika kituo cha Huduma kaunti ya Mombasa walishiriki katika zoezi la kuchangisha damu na kutoa hamasisho kwa wakazi kuhusu umuhimu wa kutoa damu. Taasisi ya utoaji damu nchini imekiri kuwa pwani inakumbwa uhaba wa damu na kuwarai wakazi kujitokeza na kutoa damu. Taasisi hiyo inasema kuwa uhaba wa damu nchini husababisha watu wengi kupoteza maisha ilhali damu inayochangishwa ingeweza kuokoa maisha. Washirika hawa wanalenga kuendeleza zoezi la kuchangisha damu katika kaunti zote za pwani.