Wafanyibiashara pwani watakiwa kuwa waangalifu dhidi ya watu wanajidai kuwa maafisa wa KEBS

  • | Citizen TV
    327 views

    Shirika la kubaini ubora wa bidhaa nchini KEBS limewatahadharisha wafanyibiashara dhidi ya matapeli wanaojifanya kuwa maafisa wa shirika hilo na ambao wanawahangaisha wafanyibiashara.visa vingi vimeripotiwa katika kaunti za Kwale na Mombasa ambapo watu wanaojitambulisha kama maafisa wa KEBS wamekuwa wakivamia biashara ndogo na kuwalaghai wafanyibiashara.