Kenya na Uganda zimetia saini mkataba wa ujenzi wa bwawa la Ang’ololo Teso Kusini

  • | Citizen TV
    761 views

    Serikali kwa ushirikiano na serikali ya Uganda zimetia saini mkataba wa maelewano kuhusu mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika mto Ang'ololo, eneo bunge la Teso south kaunti ya Busia. Bwawa hilo linalojengwa kwa kima cha shilingi bilioni kumi na nane limetajwa kama afueni kwa wakazi 300,000 wa Kenya na Uganda, ambao kwa muda mrefu wametaabika na ukosefu wa maji safi ya kunywa na ya matumizi mengine nyumbani kando na ajira vijana. Mradi huo vile vile unanuiwa kuboresha uzalishaji wa chakula kupitia kilimo cha unyunyizaji maji katika hekta 4,000 za mashamba yaliyoko katika kaunti ya Busia na maeneo ya Tororo, Namisindwa na Manafwa nchini Uganda.