Katibu katika, Idara ya Elimu na Mafunzo ya kiufundi Dkt Esther Muoria ametoa wito kwa taasisi za kiufundi kuzingatia ujuzi wa vitendo, utafiti na uvumbuzi. Akizungumza wakati wa maonyesho ya Kitaifa ya Elimu ya Ufundi Stadi, Muoria alisema kuwa hatua hii itahakikisha wanafunzi wanabuni mbinu ambazo zitawapa kipato tofauti badala ya kusubiri kuajiriwa baada ya kukamilisha masomo yao.Mkuu wa Chuo cha Kitaifa cha kiufundi Kiambu Sammy Waititu, alisema wamechukua hatua kabambe ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu katika ujuzi na uvumbuzi. Chuo hicho kilikuwa miongoni mwa taasisi za mafunzo ya ufundi stadi zilizoshiriki katika maonyesho hayo na kunyakua tuzo kadhaa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News