Serikali inatakiwa kutoa habari yakinifu kuhusiana na madai kuwa huenda kundi la Wakenya lilipelekwa ughaibuni kushiriki katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Familia tano ambazo wapendwa wao kwa sasa wamekwama ughaibuni waliliambia shirika la utangazaji humu nchini, KBC kwamba wanaamini serikali kwa hakika, inatambua kwamba wapendwa wao walisajiliwa na kupelekwa nchini Urusi kuwasaidia wanajeshi wake kwenye vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Baadhi ya familia hizo sasa zinadai wanao wamekwama ughaibuni, wakiwa hawana namna ya kurejea nyumbani. Joseph Wakhungu na taarifa hii kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive