Skip to main content
Skip to main content

Maeneo kame kaskazini mwa nchi yameathiriwa zaidi na njaa

  • | KBC Video
    233 views
    Duration: 5:45
    Yamkini watu Milioni-2 wanakabiliwa na baa la njaa huku ukame ukikithiri kwenye maeneo kame hapa nchini. Katika kaunti za Marsabit, Samburu na Isiolo, familia nyingi zinapitia kipindi kigumu cha ukosefu wa chakula, zikiishi kwa tumaini la nusu bilauri ya maziwa ya ngamia. Watoto hasa walio chini ya umri wa miaka mitano, wanawake wajawazito, wazee pamoja na watu wenye mahitaji maalum ndio wameathirika zaidi. Usiku wa leo, katika shajara yetu ya matukio ya ukame, ripota wetu Ben Chumba anatupakulia taarifa bainifu kutoka kaunti ya Marsabit, ambako baa la njaa huenda likasababisha watu kupoteza maisha ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive