Skip to main content
Skip to main content

Mshukiwa wa unajisi atiwa mbaroni Tana River

  • | KBC Video
    30 views
    Duration: 1:20
    Mwanaume wa umri wa makamo amekamatwa huko Mororo, Kaunti ya Tana River, kwa tuhuma za kumnajisi msichana wa miaka 6. Maafisa wa polisi walimnusuru mtuhumiwa kutoka mikononi mwa umati ambao ulikuwa unataka kumuadhibu kwa kitendo hicho.Wakazi wanalalamika kwamba mshukiwa amehusika kwenye vitendo sawia mara mara na wanataka apewe adhabu kali ili haki itendeke. Osman Wako, kiongozi wa jamii katika eneo hilo, alilalamikia kuongezeka kwa visa vya unyanyasaji wa watoto na mimba za utotoni katika eneo la Mororo, na kuhimiza wazazi kuwa waangalifuzaidi katika malezi ya watoto wao. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive