Wahudumu wa boda boda huko Kitengela, Kaunti ya Kajiado, kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka ishirini, wamefanya uchaguzi wa amani na kupata matokeo yasiyokuwa na pingamizi.
Kinyume na chaguzi za awali, ni waendeshaji boda boda waliojisajili kama wapiga kura pekee walioruhusiwa kupiga kura kwa kutumia nambari zao za utambulisho pamoja na kitambulisho cha kitaifa. Waendesha boda boda wanasema miongoni mwa masuala muhimu wanayotarajia kushughulikiwa na uongozi mpya ni umoja wa malengo, kutunga katiba inayolenga ustawi wa wanachama, utekelezaji wa hatua za usalama na nidhamu miongoni mwa wahudumu wote wa boda boda.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive