Tume ya huduma ya taifa ya polisi imesema kwamba bajeti iliyotengwa kwa ajili ya kuwaajiri makonstebo 10,000 wa polisi ilielekezwa kwa huduma ya taifa ya polisi, hatua iliyoathiri utekelezaji wa majukumu yake. Wakiongea walipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu utawala na usalama wa taifa, mwenyekiti wa tume hii Dkt. Amani Yuda pamoja na afisa mkuu mtendaji Peter Leley walisema shughuli ya kuajiri inayotarajiwa kuanza hivi karibuni huenda ikaathirika kutokana na mzozo baina ya pande hizo mbili kuhusiana na bajeti. Ripota wetu Abdiaziz na taarifa hii kwa kina.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive