Kama njia moja ya kuhakikisha utoshelevu wa chakula katika kaunti ya Turkana haswa wakati wa ukame, shirika la Seed savers network kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Turkana imeanzisha mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mbegu za kiasili ambazo zitakuwa zikitumika na wakulima wanaoishi kando kando ya mto Turkwell. Na kama anavyoarifu Cheboit Emmanuel wakulima zaidi ya elfu mbili kutoka shamba la Tisa Napool, Nanyee na Turkwell wanatarajiwa kunufaika na mbegu hizo.
Siku chache baada ya muungano wa upinzani kukashifu mikutano inayoendelea katika ikulu ya Rais, zaidi ya wawakilishi wadi 100 kutoka Kisii na Nyamira wameapa kufanya mikutano na Rais William Ruto katika Ikulu kwa kile wananchokitaja kama kutafutia maeneo yao maendeleo zaidi.