- 510 viewsDuration: 1:34Muungano wa wahadhiri wa vyuo vikuu nchini (UASU) umetoa ilani ya siku saba ya kuanza mgomo katika vyuo vikuu 41 vya umma kote nchini. Uasu inailaumu serikali kwa kushindwa kutekeleza makubaliano ya pamoja ya nyongeza ya mishahara. Wahadhiri wanadai malimbikizi ya tangu mwaka wa 2017 ambayo yamefikia zaidi ya shilingi bilioni 10 huku wakilalamika kuwa serikali imeshindwa kutekeleza awamu ya pili ya nyongeza ya mishahara ya mwaka 2021–2025.