- 4,798 viewsDuration: 1:18Rais William Ruto amewaonya viongozi wa upinzani dhidi ya kueneza siasa za ukabila nchini. Akiwahutubia viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Muranga, rais Ruto amesema serikali yake iko mbioni kutimiza ahadi ilizotoa na kuwa hana muda wa mzozo wa kisiasa na upinzani. Haya ni huku Naibu wake Profesa Kithure Kindiki ambaye alikutana na viongozi na wazee kutoka kaunti ya Tana River akisisitiza kuwa serikali itafanya maendeleo bila ubaguzi.