Skip to main content
Skip to main content

Ruto asisitiza ujenzi wa kanisa ikulu licha ya kusitishwa na mahakama

  • | Citizen TV
    497 views
    Duration: 1:13
    Rais William Ruto ameendelea kueleza mipango yake ya kuendelea na ujenzi wa kanisa ndani ya ikulu ya Nairobi. Akizungumza wakati wa ibada ya jumapili katika ikulu hii leo, Rais ameelezea imani ya kupanuliwa kwa sehemu hiyo ya ibada aliyoitaja kuwa ndogo kwa wanaumini wanaofika kwa ibada. Msimamo huu wa rais ukionekana kukinzana na uamuzi wa mahakama uliositisha ujenzi wowote wa maabadi hadi kesi iliyo mahakamani kupinga ujenzi huo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Jaji Chacha Mwita alitoa agizo la kusitisha ujenzi huu hadi Novemba 18 mwaka huu.