- 92 viewsDuration: 5:21Malezi ya watoto wenye mahitaji maalum ni changamoto kubwa sio tu kwa wazazi bali pia kwa jamii. Ni kutokana na hayo ambapo mashirika mbalimbali yamejikita kuhamasisha umma kuhusu namna ya kuishi na kuwashirikisha kikamilifu watu wenye mahitaji maalum. Kwa Dorcas Anyango kuwashughulikia watoto walemavu ni kama mwito kwake kwani licha ya kuwa ameajiriwa kuwahudumia, anafanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu akiamini kwamba hakuna binadamu anayestahili kutengwa ama kubaguliwa kutokana na maumbile yake. Hii leo Dorcas ndiye tunayemvisha taji la mwanamke bomba.