- 985 viewsDuration: 2:09Kongamano la mawakala wa kusafirisha wakenya ughaibuni limekamilka huko Mombasa huku wakitoa wito kwa serikali na bunge la kitaifa kubuni sheria ya kukabiliana na walaghai katika sekta hiyo. Wakiongea katika siku ya mwisho ya kongamano hilo hapo jana mjini Mombasa mwenyekiti wa muungano wa KAPEA Omar Juma Mwangala ametaka usawa baina ya mawakala katika kutoa nafasi za kazi ughaibuni ili kuhakikisha kuwa mawakala ghushi wamekabiliwa ipasavyo. Baadhi ya mawakala pia wametaka serikali kuhakikisha zoezi la kuwapiga msasa baadhi ya mawakala ili kutoa nafasi zaidi za kazi kwa wakenya ughaibuni.