Serikali ya Uganda yaeleza sababu ya viongozi 36 wa FDC kukamatwa Kenya

  • | VOA Swahili
    672 views
    Afisa wa Uhusiano na Itifaki wa shirika la Usalama wa Nje, ESO, Uganda Paul Mugisha anasema kundi la wanachama 36 wa chama cha siasa cha FDC waliorejeshwa kutoka Kenya, lilikamatwa kisumu kwa kujihusisha na vitendo vya kutia shaka ambapo walinda usalama nchini Kenya waliiarifu Uganda kuhusu kukamatwa kwa kundi hilo kabla ya kurejeshwa. Naye mmoja wa wanachama wa FDC Samule Makokha Mugenyi aliyekuwa huko Kenya alieleza usumbufu waliokutana nao wakati walipokuwa wakikamatwa. Naye makamu wa rais wa chama cha upinzani Uganda FDC, Salam Musumba alisema: Viongozi hao wametekwa, katika karne hii ya 21 wametekwa,⁣ Tutawasilisha barua yetu ya malalamiko Ubalozi wa Kenya nchini Uganda, alieleza. ⁣ "Na kuwajulisha kuhusu utekaji kinyume cha sheria na wa kikatili ⁣ Utekaji wa viongozi 36 wa chama cha FDC," makamu rais alieleza.⁣ Kwa mujibu wa uongozi wa FDC wakati wakikamatwa viongozi hao walikuwa ⁣katika Kituo cha Umma cha Uchungaji mjini Kisumu ambako walikuwa wanahudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo wa mikakati ya masuala ya siasa kwa wiki moja. ⁣ Polisi nchini Uganda walidai kwamba kundi hilo lilisafiri kati ya Julai 22 na 23 2024 kutoka maeneo mbalimbali ya Uganda hadi Kisumu, Kenya. #uganda #kenya #kisumu #fdc #upinzani #meya #kampala #polisi #ugaidi #ibrahimssemujjunganda