Maandamano ya nane nane I Maafisa wa usalama washika doria Mombasa

  • | KBC Video
    49 views

    Biashara nyingi katika eneo la kati kati ya mji wa Mombasa ziliendelea barabara mchana kutwa huku chache zikifungwa kutokana na hofu ya maandamano. Usalama uliimarishwa mjini humo maafisa wa polisi wakishika doria kwa kutembea na wengine wakitumia magari. Hayo yanajiri huku kundi moja la kutetea haki za binadamu katika eneo la Pwani likikosoa vikali kuwepo kwa maafisa wengi wa usalama na mikakati iliyowekwa kudumisha usalama likisema hatua hiyo iliwatia wasiwasi wananchi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News