Meya aeleza sababu ya kushindwa kusitisha utupaji takataka Kiteezi

  • | VOA Swahili
    566 views
    Meya wa Kampala, Elias Lukwago, anaeleza janga hili limetokea kwa sababu ya wale walioweka vikwazo "tulipokuwa tunaelekea katika utekelezaji wa mapendekezo yetu ya kuwa na sera ya kugeuza takataka kuwa nishati ili tuweze kusitisha utupaji takataka katika dampo hili". Vyanzo vya habari vinaeleza dampo la takataka katika eneo hili ambalo linafahamika kama Kiteezi, ambako kwa miongo mingi limekuwa likitupwa takataka zinazo zalishwa mjini Kampala, hadi kugeuka na kuwa mlima, huku wakazi waishio karibu wakilalamika kutokana na taka zenye sumu, pamoja na uharibifu wa mazingira. Polisi wa Uganda walisema Jumapili kuwa idadi ya vifo kutokana janga la maporomoko ya takataka katika dampo hilo mjini Kampala ilifikia 21, wakati timu za uokozi zikiendelea kutafuta manusura na idadi ya miili inayopatikana ikielekea kuongezeka.⁣ - Reuters, AP, VOA⁣ Picha na Mwandishi wa VOA, Sadam Muballe, Kampala, Uganda.⁣ ⁣ ⁣ #uganda #kampala #takataka #dumpo #maporomoko #vifo #polisi #voa #voaswahili