Wizara ya Afya yataka kaunti kuweka mikakati kuzuia mchemko wa ugonjwa wa Mpox

  • | Citizen TV
    228 views

    Wizara ya afya imezitaka serikali za kaunti kuweka mikakati ya kuwatenga wagonjwa wa mpox kama ilivyokuwa wakati wa janga la covid-19. Katibu wa afya ya umma mary muthoni amesema kuwa serikali kuu itashirikiana na serikali z akaunti kuweka mikakati kabambe ili kukabili maambukizi ya ugonjwa huo ambao umetajwa kuwa dharura na shirika la afya duniani. Muthoni amesema kuwa wizara ya afya imefungua kituo cha dharura na vituo vingine 25 ambavyo vitasaidia kuweka uangalizi wa maambukizi zaidi.