Waziri Joho awasilisha vyeti kwa wavuvi huko Kisumu

  • | Citizen TV
    703 views

    Waziri wa madini na uchumi wa majini Ali Hassan Joho ameahidi kushirikiana na wizara ya ardhi, ili kutoa vyeti vya umiliki kwa makundi ya wavuvi katika ufuo wa ziwa victoria_ Akizungumza katika ufuo wa Ogal kaunti ya Kisumu, Joho alisema kuwa unyakuzi wa ardhi kwenye ufuo wa ziwa hilo kumechangia pakubwa kudorora kwa hadhi ya wavuvi, kwani serikali haiwezi kuunda miundombinu katika ardhi yenye utata. Serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni 1.4 kuimarisha miundombinu katika fuo tisa za ziwavictoria. Ujenzi huo unatarajiwa kutoa nafasi bora kwa wavuvi kuhifadhi samaki na kuuza katika soko za nje ili kuimarisha mapato yao.