Wazee wa jamii Mlima Kenya watahadharisha kuhusu migawanyiko

  • | KBC Video
    17 views

    Baadhi ya wazee wa jamii ya Agikuyu katika kaunti ya Kiambu wamewashutumu viiongozi waliochaguliwa katika eneo la Mlima Kenya kwa madai ya kuibua mgogoro baina ya naibu rais Rigathi Gachagua na waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki.Wakigusia kile kilichotajwa kuwa Azma ya Nyahururu ambapo wabunge 48 kutoka eneo la Mlima Kenya walidhamiria kumtawaza Kindiki kuwa kiungo kati ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na serikali ya kitaifa, wazee hao walitahadharisha kwamba siasa za ubabe zinahujumu utoaji huduma kwa wananchi. Waliwataka wabunge kuzingatia majukumu yao ya utungaji sheria na kutathmnini utendakazi wa serikali badala ya kujihusisha na siasa za migawanyiko.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive