Familia moja inalilia haki kuhusu kifo cha mwana wao shuleni Friends School Kamusinga

  • | Citizen TV
    1,876 views

    Familia moja kaunti ya Siaya inalilia haki baada ya mwana wao kuaga dunia kwa njia tatanishi akiwa shuleni. Familia hiyo inashutumu usimamizi wa shule ya upili ya Friends School Kamusinga kwa utepetevu wanaodai ulisababisha mwana wao kutumbukia kwenye shimo la choo na kufariki. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, familia hiyo pia inadai kufichwa kuhusu kilichosababisha kifo cha mwana wao.