Mwili wa marehemu naibu gavana wa Lamu Rapheal Munywa wawasili nyumbani

  • | Citizen TV
    988 views

    Mwili wa Marehemu Naibu Gavana wa Lamu Rapheal Munywa umewasili nyumbani kwake Mpeketoni, kaunti ya Lamu. Ibada ya wafu itafanyika katika uwanja wa Muungamo kabla ya mazishi kufanyika siku ya Alhamisi. Gavana wa Lamu issa Timami ameongoza maombolezo akisema kuwa siasa hazitaruhusiwa kwenye ibada na mazishi na kuwa atachukuwa muda wa kutosha kumteua naibu gavana atakayeweza kujaza pengo lililoachwa na Munywa. Viongozi waliokuwepo walimtaja kama amchapa kazi. Munywa alifariki katika hospitali ya Nairobi ambako alikuwa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa miezi miwili.