Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli asistiza kuwa hatashurutishwa

  • | Citizen TV
    7,261 views

    Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli amezidisha ukaidi akisistiza kuwa hatashurutishwa na yeyote kutekeleza majukumu yake ambayo ni pamoja na kuwaajiri, kuwatuma na kuwaondoa maafisa wa polisi. Masengeli amesema kuwa idara ya polisi ni idara huru na ina majukumu ya kuhakikisha kuwakila mkenya anapewa ulinzi. Licha ya masengeli kusema kuwa tayari jaji lawrence mugambi amerejeshewa ulinzi, tume ya huduma za mahakama JSC imesema kuwa haina thibitisho kuhusu madai ya masengeli. Na kama anavyoarifu Ben Kirui, mashirika mbalimbali yanamtaka masengeli kuwajibishwa.