Junior Starlets kufanyia matayarisho ya mwiaho kwa Kombe la Dunia nchini Uhispania

  • | Citizen TV
    197 views

    Timu ya taifa ya Kenya ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ilifanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuondoka kwenda Uhispania siku ya Alhamisi. Junior Starlets watapiga kambi nchini Uhispania kwa siku 11 kabla ya kuelekea Jamhuri ya Dominika mnamo Oktoba mosi. Kocha Mildred Cheche anasema kambi hiyo ya Uhispania inajiri wakati muafaka baada ya benchi la ufundi kuimarisha maeneo kadhaa ambayo yalikuwa na upungufu wakati wa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia. Timu hiyo itakuwa nchini Uhispania kwa siku 11 ambapo watakuwa na kambi ya mazoezi na kucheza mechi kadhaa za kirafiki na timu za Uhispania. Kambi hiyo pia itatumika kuimarisha ujasiri wa wachezaji kabla ya kibarua kikubwa katika Jamhuri ya Dominika. Timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 ni timu ya kwanza ya Kenya kufuzu kwa kombe lolote la dunia la FIFA.