Serikali ya kaunti ya Busia yatafuta mbinu ya kuboresha lishe miongoni mwa wakazi na wanafunzi

  • | Citizen TV
    90 views

    Serikali ya kaunti ya Busia kupitia idara za elimu, kilimo na afya imeanzisha ushirikiano na washikadau mbalimbali ili kutafuta mbinu ya kuboresha lishe miongoni mwa wakazi na wanafunzi mbali na kupunguza visa vya kudumaa. Mpango huo unanuia kuhakikisha kwamba wenyeji wanakuza na kupata vyakula vyenye virutubishi ikizingatiwa kwamba asilimia 15 ya watoto Busia wamedumaa.