Mahakama kuu yaamua kuwa hazina ya NG-CDF imekiuka katiba

  • | Citizen TV
    271 views

    Mahakama kuu imeamua kuwa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge imekiuka katiba. Majaji wawili Kanyi Kimondo na Roselyne Aburili kati ya watatu waliamua kuwa hazina hiyo inakiuka taratibu za usimamizi na uwajibikaji wa fedha. Jaji Mugure Thande pekee ndiye alikuwa na maoni kinzani. Katika hukumu hiyo mahakama pia imesema kwamba baadhi ya majukumu ya wabunge chini ya hazina hiyo ni ya serikali za kaunti.