Naibu Gachagua awapa changamoto wabunge wanaopanga kumngo’a mamlakani

  • | K24 Video
    424 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua sasa amewapa changamoto wabunge wanaopanga kumngo’a mamlakani akiwataka washughulike na kazi ya kutunga sheria zinazowanufaisha wakenya. Akizungumza alipozuru kaunti za eneo la mlima kenya Gachagua alimtaka rais William Ruto kumuacha afanye kazi aliyopigiwa kura na wananchi akisema kuwa ikiwa rais atachagua mtu mwingine mwaka wa elfu mbili ishirini na saba atakubali ila kwa sasa aachwe amalize kipindi hiki. Gachagua amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayemtoa mamlakani kama sio wananchi waliompigia kura akitaka rais Ruto akome kutumia wabunge kumtimua.