Naibu Rais Gachagua adaiwa kumpuuza Rais William Ruto

  • | Citizen TV
    3,184 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua alitumia muda wa saa moja na dakika hamsini kutoa utetezi wake katika bunge la kitaifa hapo jana. Katika muda huo, gachagua alipinga madai yote dhidi yake katika hoja ya kumuondoa mamlakani. Gachagua alitofautiana na kauli kuwa amewakosea heshima wabunge, amemdhalilisha rais na kuwadharau viongozi wanawake. Gachagua alitumia video za Rais Ruto kutoa utetezi wake.