Awamu ya pili ya uchaguzi wa UDA nyanjani kuandaliwa mwezi ujao

  • | KBC Video
    24 views

    Chama cha UDA kimetangaza awamu ya pili ya uchaguzi mashinani, utakaoandaliwa kati ya tarehe 11 na 12 mwezi Aprili mwaka huu katika kaunti 22. Mwenyekiti wa chama hicho Cecily Mbarire akitangaza hayo aliwahimiza wawaniaji wote kujisajili,akisema kuwa mchakato wa usajili umefunguliwa hadi tarehe 21 mwezi huu . Wagombeaji wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya chama hicho UDA.ke. Chama kufikia sasa kimenunua zaidi ya vifaa 10,000 vya uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unaadaliwa kupitia mfumo wa kielektroniki ili kuhakikisha kwamba unakuwa wazi, huru na wa haki.Chama hicho hadi sasa kimefanikiwa kufanya chaguzi katika kaunti 5.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News