- 560 viewsDuration: 36sWaakilishi wa kenya kwenye mchuano wa CECAFA kuwania kufuzu kwa kombe la klabu bingwa Afrika upande wanawake Police Bullets fc wameingia nusu fainali kufuatia ushindi wa mbili bila dhidi ya Den Den fc ya Eritrea alasiri ya leo.kwenye mechi iliyochezwa uwanjani nyayo hapa Nairobi, Bullets waliandikisha mabao yote kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Emily Moranga na Zaina Namuleme. Wasichana hao chini ya kocha beldine Odemba sasa watasubiri kujua mpinzani wao wakilenga tiketi ya pekee kwenye mchuano huo uliokuwa na timu tisa.