Chama cha labour chashinda uchaguzi mkuu Uingereza

  • | Citizen TV
    1,789 views

    Chama cha labour kimeshinda rasmi uchaguzi mkuu wa uingereza baada ya kutwaaviti 326 vinavyohitajika. Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema kuwa anakubali kushindwa kwa chama cha Conservative. Aidha Waziri Mkuu mtarajiwa Keir Starmer anayekiongoza chama cha Labour kilichopata ushindi mkubwa na ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Sunak kama Waziri Mkuu wa Uingereza amesema kuwa mabadiliko uingereza yanaanza sasa. Sunak ametaja matokeo ya uchaguzi huo kama uamuzi wa kutisha na kuongeza kuwa kuna mengi ya kujifunza kutokana na uchaguzi huo. Chama cha Labour kinatarajiwa kuunda serikali ijayo