Cheptumo na Ruku waidhinishwa kuwa mawaziri

  • | KBC Video
    92 views

    Hannah Cheptumo na Geoffrey Ruku wameidhinishwa kwa nyadhifa za mawaziri kwenye wizara za jinsia na utumishi wa umma mtawalia. Hii ni baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha uteuzi wao. Wabunge hata hivyo walielezea kukerwa na matamshi ya Cheptumo ambaye alinukuliwa akidai kwamba baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wanauawa katika vyumba vya malazi ya muda wakitafuta pesa. Huku hayo yakijiri, hatma ya Stephen Isaboke aliyeteuliwa kwa wadhifa wa katibu katika wizara ya utangazaji na mawasiliano haijabainika, wabunge wakihofia mkinzano wa maslahi katika uteuzi huo. Ripota wetu Abdiaziz Hashim, ma maelezo zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive